Mithali 28

Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.

Proverbs 28:5 (UKJV) Evil men understand not judgment: but they that seek the LORD understand all things.

3Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao.

4Wale waiachao sheria huwasifu waovu, bali wale waishikao sheria huwapinga.

5Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.

6Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.

7Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.