8Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.
9Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
10Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
11Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.
12Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu.