19Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, ajapoelewa, hataitikia.
20Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.
21Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni.
22Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi.
23Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.