Mithali 29

Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.

Proverbs 29:4 (UKJV) The king by judgment establishes the land: but he that receives gifts overthrows it.

2Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.

3Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.

4Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.

5Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake.

6Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.