8Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.
9Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘Bwana ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.
10“Usimchongee mtumishi kwa bwana wake, asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo.
11“Wako watu wale ambao huwalaani baba zao na wala hawawabariki mama zao;
12wale ambao ni safi machoni pao wenyewe kumbe hawakuoshwa uchafu wao;