27Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.
28Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme.
29“Viko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao, naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha:
30simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, asiyerudi nyuma kwa chochote;
31jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu, naye mfalme pamoja na jeshi lake lililomzunguka.