5“Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.
6Usiongeze kwenye maneno yake, ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.
7“Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana; usininyime kabla sijafa:
8Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.
9Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘Bwana ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.