15Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu kwa watumishi wake wa kike.
16Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.
17Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.
18Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku.
19Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.