17Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.
18Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku.
19Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.
20Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.
21Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.