1Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:
2“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu, ee mwana wa nadhiri zangu,
3Usitumie nguvu zako kwa wanawake, uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.
4“Ee Lemueli, haifai wafalme, haifai wafalme kunywa mvinyo, haifai watawala kutamani sana kileo,
5wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa.