17Wanakula mkate wa uovu, na kunywa mvinyo wa jeuri.
18Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.
19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae.
20Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia; sikiliza kwa makini maneno yangu.
21Usiruhusu yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako;