18Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.
19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae.
20Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia; sikiliza kwa makini maneno yangu.
21Usiruhusu yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako;
22kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili wote wa mwanadamu.