Mithali 4

Usiruhusu yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako;

Proverbs 4:21 (UKJV) Let them not depart from yours eyes; keep them in the midst of yours heart.

19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae.

20Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia; sikiliza kwa makini maneno yangu.

21Usiruhusu yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako;

22kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili wote wa mwanadamu.

23Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.