28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka bila miguu yake kuungua?
29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.
30Watu hawamdharau mwizi kama akiiba kukidhi njaa yake wakati ana njaa.
31Pamoja na hayo, kama akikamatwa, lazima alipe mara saba, ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.
32Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.