23mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.
24Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo.
25Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake.
26Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa.
27Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.