2Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
3Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako.
4Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako;
5watakuepusha na mwanamke mzinzi, kutokana na mwanamke mpotovu na maneno yake ya kubembeleza.
6Kwenye dirisha la nyumba yangu nilitazama nje kupitia upenyo kwenye mwimo wa dirisha.