12“Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; ninamiliki maarifa na busara.
13Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu.
14Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu.
15Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki,
16kwa msaada wangu wakuu hutawala, na wenye vyeo wote watawalao dunia.