14Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu.
15Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki,
16kwa msaada wangu wakuu hutawala, na wenye vyeo wote watawalao dunia.
17Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
18Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri udumuo na mafanikio.