22“Bwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake, kabla ya matendo yake ya zamani;
23niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.
24Wakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa, wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji;
25kabla milima haijawekwa mahali pake, kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa,
26kabla hajaumba dunia wala mashamba yake au vumbi lolote la dunia.