23niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.
24Wakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa, wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji;
25kabla milima haijawekwa mahali pake, kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa,
26kabla hajaumba dunia wala mashamba yake au vumbi lolote la dunia.
27Nilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake, wakati alichora mstari wa upeo wa macho juu ya uso wa kilindi,