1Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti?
2Juu ya miinuko karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo;
3kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema:
4“Ni ninyi wanaume, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.
5Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili; ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu.