29wakati aliiwekea bahari mpaka wake ili maji yasivunje agizo lake, na wakati aliweka misingi ya dunia.
30Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake. Nilijazwa na furaha siku baada ya siku, nikifurahi daima mbele zake,
31nikifurahi katika dunia yake yote nami nikiwafurahia wanadamu.
32“Basi sasa wanangu, nisikilizeni; heri wale wanaozishika njia zangu.
33Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima; msiyapuuze.