31nikifurahi katika dunia yake yote nami nikiwafurahia wanadamu.
32“Basi sasa wanangu, nisikilizeni; heri wale wanaozishika njia zangu.
33Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima; msiyapuuze.
34Heri mtu yule anisikilizaye mimi, akisubiri siku zote malangoni mwangu, akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu.
35Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana.