5Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili; ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu.
6Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema; ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa.
7Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu.
8Maneno yote ya kinywa changu ni haki; hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi.
9Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi; hayana kasoro kwa wale wenye maarifa.