4Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa!
5Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya.
6Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
7“Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi.
8Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda.