12Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge.
13Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? Kwa nini anajiambia mwenyewe, “Hataniita nitoe hesabu?”
14Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima.
15Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana.
16Bwana ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake.