10Mateka wake hupondwa, huzimia; wanaanguka katika nguvu zake.
11Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.”
12Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge.
13Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? Kwa nini anajiambia mwenyewe, “Hataniita nitoe hesabu?”
14Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima.