9Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake.
10Mateka wake hupondwa, huzimia; wanaanguka katika nguvu zake.
11Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.”
12Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge.
13Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? Kwa nini anajiambia mwenyewe, “Hataniita nitoe hesabu?”