Zaburi 10

Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

Psalm 10:2 (UKJV) The wicked in his pride does persecute the poor: let them be taken in the devices that they have imagined.

1Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida?

2Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

3Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana Bwana.

4Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.