Zaburi 102

Ee Bwana, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.

Psalm 102:1 (UKJV) Hear my prayer, O LORD, and let my cry come unto you.

1Ee Bwana, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.

2Usinifiche uso wako ninapokuwa katika shida. Unitegee sikio lako, ninapoita, unijibu kwa upesi.

3Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi, mifupa yangu inaungua kama kaa la moto.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.