12kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
13Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;
14kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.
15Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, anachanua kama ua la shambani;
16upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, mahali pake hapalikumbuki tena.