6Bwana hutenda haki, naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.
7Alijulisha Mose njia zake, na wana wa Israeli matendo yake.
8Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.
9Yeye hatalaumu siku zote, wala haweki hasira yake milele,
10yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.