14Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini:
15divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu.
16Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
17Humo ndege hufanya viota vyao, korongo ana nyumba yake kwenye msunobari.
18Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu, majabali ni kimbilio la pelele.