20Unaleta giza, kunakuwa usiku, wanyama wote wa mwituni huzurura.
21Simba hunguruma kwa mawindo yao, na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.
22Jua huchomoza, nao huondoka, hurudi na kulala katika mapango yao.
23Kisha mwanadamu huenda kazini mwake, katika kazi yake mpaka jioni.
24Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako.