26Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake.
27Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake.
28Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema.
29Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini.
30Unapopeleka Roho wako, wanaumbwa, nawe huufanya upya uso wa dunia.