Zaburi 104

Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake.

Psalm 104:27 (UKJV) These wait all upon you; that you may give them their food in due season.

25Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.

26Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake.

27Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake.

28Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema.

29Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.