7Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka,
8yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia.
9Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena.
10Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima.
11Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao.