5Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa.
6Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima.
7Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka,
8yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia.
9Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena.