9Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena.
10Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima.
11Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao.
12Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, huimba katikati ya matawi.
13Huinyeshea milima kutoka orofa zake, dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake.