11“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”
12Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake,
13walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
14Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
15“Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”