13walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
14Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
15“Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”
16Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote,
17naye akatuma mtu mbele yao, Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa.