16Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote,
17naye akatuma mtu mbele yao, Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa.
18Walichubua miguu yake kwa minyororo, shingo yake ilifungwa kwa chuma,
19hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, hadi neno la Bwana lilipomthibitisha.
20Mfalme alituma watu wakamfungua, mtawala wa watu alimwachia huru.