1Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
2Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu.
3Lishangilieni jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
4Mtafuteni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.