27Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao, miujiza yake katika nchi ya Hamu.
28Alituma giza na nchi ikajaa giza, kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?
29Aligeuza maji yao kuwa damu, ikasababisha samaki wao kufa.
30Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.
31Alisema, yakaja makundi ya mainzi, na viroboto katika nchi yao yote.