29Aligeuza maji yao kuwa damu, ikasababisha samaki wao kufa.
30Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.
31Alisema, yakaja makundi ya mainzi, na viroboto katika nchi yao yote.
32Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe, yenye umeme wa radi nchini yao yote,
33akaharibu mizabibu yao na miti ya tini, na akaangamiza miti ya nchi yao.