5Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,
6enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7Yeye ndiye Bwana Mungu wetu, hukumu zake zimo duniani pote.
8Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
9agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.