7Yeye ndiye Bwana Mungu wetu, hukumu zake zimo duniani pote.
8Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
9agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.
10Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele:
11“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”