1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele.
2Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui,
3wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini.