Zaburi 107

Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.

Psalm 107:12 (UKJV) Therefore he brought down their heart with labour; they fell down, and there was none to help.

10Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, wafungwa wakiteseka katika minyororo,

11kwa sababu walikuwa wameasi dhidi ya maneno ya Mungu na kudharau shauri la Aliye Juu Sana.

12Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.

13Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.

14Akawatoa katika giza na huzuni kuu na akavunja minyororo yao.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.