18Wakachukia kabisa vyakula vyote, wakakaribia malango ya mauti.
19Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.
20Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo yao.
21Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.
22Na watoe dhabihu za kushukuru, na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.